
Taarifa za ndani toka chombo kimoja cha ndani nchini Italia kimeripoti kuwa aliyekuwa bosi wa Liverpool Rafa Benitez huenda akajiunga na klabu ya Rossoneri au AC Milan muda wowote kuanzia sasa.Milan wameanza vubaya msimu huu wa Ligi kwani tayari wameshapoteza mechi 2 kati ya tatu za Serie A na jana wakianza kwa sare ya bila kufungana dhidi ya klabu ya Anderlecht ya nchini Ubelgiji katika Ligi ya mabingwa Ulaya.Benitez anakumbwa sana na mashabiki wa Liverpool kutokana kuiwezesha klabu hiyo kuutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 2005.Pamoja na hayo kocha huyo amewahi kuifundisha klabu hasimu ya AC Milan naizungumzia Inter Milan mwaka 2010/11.Kuja kwa Benitez kunamaanisha ndoa ya Milan na Allegri ambaye ndiye kocha wa Milan ipo karibu kuvunjika
0 comments:
Post a Comment