Yanga ambayo imerudisha makali yake katika kinyanganyiro cha Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania bara, imefikisha jumla ya pointi 23 sawa na
Simba SC ambao wanaongoza ligi kwa tofauti ya mabao ya kufungana
kufungwa.
Yanga ilianza mbio za kusaka point 3
muhimu na katika sekunde ya 15 ya mchezo, Mshambuliaji Saimon Msuva
alikosa bao la wazi baada ya kupewa pasi nzuri na Haruna Niyonzima,
lakini Msuva alishindwa kuukwamisha mpira huo wavuni.
Dakika
ya 2 ya mchezo, Nadri Haroub 'Cannavaro' Saimonaliipatia Yanga bao la
kwanza kwa kichwa, akiunganisha mpira wa faulo uliopigw ana Athuman Idd
baada ya mshambuliaji Didier Kavumbagu kuchezewa ndivyo sivyo nje kidogo
ya eneo la hatari.
Saimon Msuva, Hamis Kiiza na
Haruna Niyonzima walikos amabao mengi ya wazi katika kipindi cha kwanza
kutokana na kutokua makini katika umaliziaji hali iliyopelekea mpaka
dakika 30 za mchezo Yanga kuendelea kuwa mbele kwa bao 1 tu.
Didier
Kavumbagu aliipatia Yanga bao la pili katika dakika ya 39 baada ya
kumalizia pasi nzuri iliyopigwa na mshambuliaji Hamis Kiiza na kumkuta
mfungaji ambaye hakufanya ajizi na kuukwamisha mpira huo wavuni.
Wachezaji
wa timu ya Yanga waliendelea kuutawala mchezo kwa dakika zote za
kipindi cha kwanza na kama umaliziaji ungekuwa makini basi Yanga
ingeibuka na ushindi mkubwa zaidi katika dakika 45 za kipindi cha
kwanza.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza Young Africans 2-0 Mgambo JKT.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko kwa kumuingiza Kelvin
Yondani aliyekuwa majeruhi kwa mda mrefu kuchukua nafasi ya Shadrack
Nsajigwa.
Mabadiliko hayo yalileta uhai kwa vijana
wa Jangwani kwani Mbuyu Twite ambaye alirudi kucheza nafasi ya mlinzi
wa kulia, alipata nafasi ya kupanda kuongezangvu mashambulizi hali
iliyopelekea walinzi wa Mgambo JKT kumchezea faulo nyingi sana.
Jeryson
Tegete ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Didier Kavumbagu aliipatia
Yanga bao la tatu baada ya kumalizia krosi safi iliyopigwa na Oscar
Joshua aliyepanda kuongeza nguvu mashambulizi na kumkuta Tegete alifunga
kwa kupiga shuti kali na mpira kuingia sehemu ya nyavu ndogo za juu.
Kama
washambuliaji wa Yanga wangekuwa makini wangeweza kufunga mabao mengi
zaidi, lakini umakini wao katika umaliziaji wa Saimon Msuva, Hamis Kiiza
na Haruna Niyonzima uliwafanya wasiweze kupata mabao mengine ya ziada
kwani nafasi walizozipata zingeweza kuifanya Yanga iondoke na ushindi
mnono.
Mpaka dakika 90 za mchezo za mwamuzi Martin Sanya zinamalizika, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 Mgambo JKT
Yanga
inajiandaa na mchezo wake dhidi ya Azam Fc siku jumapili, pambano
ambalo litafanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Yanga:
1.Ally Mustapha, 2.Shadrack Nsajigwa/Klevin Yondani, 3.Oscar Joshua,
4.Nadir Haroub, 5.Mbuyu Twite, 6.Athuman Idd, 7.Saimon Msuva, 8.Frank
Domayo/Nurdin Bakari 9.Didier Kavumbagu/Jeryson Tegete, 10.Hamis Kiiza,
11.Haruna Niyonzima